Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars, ametangaza kikosi rasmi kitakachoshiriki mashindano ya FIFA Series 2026, huku majina ya nyota wanaokipiga katika Ligi Kuu ya NBC nchini Tanzania yakivutia macho ya wengi.
Katika orodha hiyo, kiungo fundi wa Young Africans, Duke Abuya, na mshambuliaji chipukizi wa Simba SC, Mohammed Bajaber, wamejumuishwa kufuatia viwango bora walivyoonyesha kwenye klabu zao msimu huu.
Kikosi hicho kimechanganya uzoefu na damu changa, kikiongozwa na nahodha na mshambuliaji tegemeo Michael Olunga (Al Arabi). Safu ya ulinzi itaimarishwa na nyota kama Zak Vyner anayecheza nchini Uingereza (Wrexham) na Rooney Onyango (Sogndal), wakati safu ya kiungo ikiwa na mafundi kama Richard Odada na Manzur Suleiman anayecheza nchini Ufaransa (Stade De Reims).
Uteuzi wa Bajaber na Abuya unathibitisha kukua kwa ushindani katika ligi ya Tanzania na jinsi inavyotoa nafasi kwa wachezaji kuonekana katika anga za kimataifa.
Kikosi kamili kilichotajwa ni kama ifuatavyo:
Makipa: Byrne Omondi, Brian Bwire, Ian Otieno.
Walinzi: Frank Odhiambo, Abud Omar, Sylvester Owino, Zak Vyner, Rooney Onyango, Daniel Sakari.
Viungo: Alpha Onyango, Duke Abuya (Yanga), Richard Odada, Chris Erambo, Manzur Suleiman.
Washambuliaji: Austine Odhiambo, William Lenkupae, Job Ochieng, Mohammed Bajaber (Simba SC), Zech Obiero, Clarke Oduor, Michael Olunga, Ryan Ogam, Lawrence Okoth.

