Mnamo mwaka 2019, CAF iliitaka Espérance Sportive de Tunis kurejesha medali na kombe lao la ushindi wa CAF Champions League baada ya rufaa iliyowasilishwa na klabu ya Morocco, Wydad Casablanca.
Hii ilitokea kwa sababu Wydad walitoka uwanjani wakipinga maamuzi ya mwamuzi, na walikataa kurudi licha ya Rais wa CAF kuwaomba kwa takriban saa mbili; hivyo mchezo ukahesabiwa kuwa wamepoteza, na Esperance wakatangazwa washindi awali.
Hata hivyo, Esperance walipeleka kesi hiyo katika Court of Arbitration for Sport (CAS) kupinga uamuzi wa CAF, wakashinda rufaa hiyo, na wakabaki kuwa mabingwa halali.
