Afisa Habari wa Young Africans, Ally Kamwe, ametoa malalamiko mazito dhidi ya wapinzani wao Simba SC, akidai kuwa mambo mengi yasiyo ya michezo yalitawala kuelekea kupatikana kwa sare ya 0-0 katika dabi iliyopita. Kamwe amedai kuwa kulikuwa na matukio ya utata ya uamuzi pamoja na vitendo vya ushirikina ambavyo viliisaidia Simba kupata alama hiyo moja.
Katika andiko lake, Ally Kamwe amefunguka yafuatayo:
"Kwanza ilikuwa OFFSIDE.. Pili, AKASHIKA. Move ikaruhusiwa kuendelea kama hakijatokea kitu. Sitaki kabisa kukumbusha kuwa Mchezaji huyu alitakiwa kufungiwa MECHI 5 kwa kosa la kumpiga kiwiko mchezaji wa Dodoma Jiji ... Sitaki kuwakumbusha, kuwa Waamuzi walishatishiwa kufungiwa Maisha kimpira na kupelekwa JELA kuhusu mechi hii.
Turidi uwanjani, Watu hawa baada ya mazoezi ya mwisho siku moja kabla ya mchezo, wakagoma kuondoka uwanjani Usiku.. Wakafanya Ushirikina na vurugu za kila aina.. Wakaja kutolewa kwa msaada wa Polisi.
Hawakumaliza, Siku ya mechi wametumia mlango wa VVIP kuingia uwanjani. Wakavunja mlango wa chumba cha Waandishi wa Habari. Muda wa Pitch Feeling, wakautumia kuzunguka uwanja na kufanya vitendo vya Kishirikina bila wasiwasi wote.
Hapa Najaribu kuwaonyesha kwa uchache tu NGUVU iliyotumika hadi Makolo wamepata POINTI 1 kwenye Derby. Kimsingi, kwa mtu anayejua Mpira vizuri atakubaliana na mimi.. JANA SIMBA wamethibitisha ni WADOGO SANA KWA YANGA na watatumia miaka mingi sana kuja kushinda Derby.
Nguvu yote kubwa sana Ilitumika ndani na nje ya uwanja haijaweza kufuta Uteja wao. Wana kikosi chenye wachezaji machachari na Viongozi wenye mihemko. Kama isingekuwa mambo ya kupelekana JELA, ikapigwa FAIR, Prince Dube angewaveka ile chuma ndio mngeona mengi zaidi jana...
Wanazuga Kulalamika na kutukana watu leo ili kuficha Vitu vya hovyo walivyofanya na Wameshindwa kupata Ushindi .. Hii inawauma sana. KULIWA MARA 6 Imebaki pale pale na POINTI 5 ZIMESIMAMA VILEVILE." Ameandika Ali Kamwe. msemaji wa Yanga SC.
