Afisa Habari wa klabu ya Singida Black Stars, Hussein Massanza, amemsifia vikali mkandarasi aliyejenga uwanja wao wa Airtel uliopo Singida.
*Wakati tunajenga Airtel Stadium, tulimwelekeza mkandarasi jambo moja muhimu sana: hata inyeshe mvua ya mawe, hakikisha maji hayatuami uwanjani na mechi inaweza kuchezwa katika hali yoyote ya hewa.
Tunafurahi mkandarasi alituelewa na alifanya kazi yake kwa asilimia 100.
Kwa bahati mbaya, bado viwanja vingi nchini vinapata changamoto ya kuhimili mabadiliko ya hali ya hewa, hasa nyakati za mvua. Wakati mwingine mechi hulazimika kuahirishwa.
Lakini ukweli ni kwamba mvua ni baraka; katika dunia ya sasa haipaswi tena kuonekana kama kero kwa mpira wa miguu.
Tunawakaribisha wamiliki wa viwanja kuja kujifunza kwetu kuhusu ujenzi wa miundombinu ya kisasa ya viwanja.
Kwa sasa, timu zote zinazoathirika na hali ya viwanja zinakaribishwa kukodisha Airtel Stadium. Tunachaji bei za kizalendo kabisa!" Alimaliza Massanza



