Mshambuliaji wa Coastal Union, Adam Salamba, ameripotiwa kujiweka kando na kikosi cha ‘Wagosi wa Kaya’ kutokana na kile kinachodaiwa kuwa ni kutokamilishiwa kiasi cha fedha zake za usajili.
Inaelezwa kuwa Salamba, aliyejiunga na timu hiyo Agosti 1, 2025, ameshaondoka kambini na hatakuwa sehemu ya kikosi kitakachochuana na Simba Aprili 2, 2026, hadi hapo stahiki zake zitakapolipwa.
Hata hivyo uongozi wa Coastal Union umekiri kuwepo kwa deni hilo na kusema mchakato wa kumlipa unaendelea, huku wakitamani mchezaji huyo angeendelea na mazoezi wakati taratibu zikikamilishwa.
Salamba amewahi kuzitumikia klabu kadhaa ikiwemo Simba, Namungo, na Stand United, pamoja na kucheza soka la kulipwa nchini Libya, Misri, na Kuwait.
