Yanga wako kwenye nafasi nzuri ya kumsaini kipa wa Pamba Jiji,Yona Amosi (26).
Yanga wameahidi kuwapa Pamba Jiji golikipa mwingine na kiasi cha pesa,wakati huo Simba na Singida waliulizia upatikanaji wa kipa huyo kabla ya michuano ya Mapinduzi kuanza,ila hadi sasa hawajapeleka ofa rasmi.
Yona Amos,amebakiza mkataba wa miezi (6) na Pamba,na tayari amewambia wamuuze January hii kwani mwishoni mwa msimu hatosaini mkataba mpya.
Yanga wanamtaka Yona kuziba nafasi ya Khomein Abubakar.
