MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza

AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika.

Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika.

Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.


Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote.

Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika.

Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Klabu bingwa Afrika mwaka 1974.

Ikumbukwe Simba iliweka historia mwaka 1974 pale ilipofanikiwa kuingia nusu fainali ya Afrika, hasa baada ya kuitoa Heart of OAK ya Nigeria na kutinga hatua hiyo.

Wekundu hao wa Msimbazi waliamua kupambana kufa na kupona ili angalau waweze kuwajibu mahasimu wao Yanga, ambao mwaka 1968 walifanikiwa kuingia robo fainali ya michuano ya Klabu bingwa Afrika.

Ikumbukwe katika hatua hiyo ya robo fainali Yanga ilicheza na timu ya Asante Kotoko ya Ghana na kufikia mshindi kupatikana kwa kurushwa shilingi na hasa baada ya timu hizo kutoshana nguvu kwa kutoka sare.  

Hivyo Simba nao wakiwa na kikosi kilichosheheni wachezaji bora hapa nchini kwa wakati huo, kiliweza kupambana na kufanikiwa kuingia nusu fainali na kuizidi Yanga iliyoishia kucheza robo fainali. 

Kitendo cha Yanga kuingia nusu fainali ya kombe la Shirikisho Afrika, Ally Kamwe asitake kuharibu rekodi ya mpira wa Afrika, kwani Simba ilikuwa klabu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya michuano ya Klabu bingwa Afrika, na rekodi hiyo haiwezi kufutika kwenye uso wa dunia. 

Hata kama Shirikisho la soka barani Afrika limeshindwa kuhifadhi kumbukumbu hizo kwenye mtandao sababu teknolojia hiyo nyakati hizo hazikuwepo,.

Lakini kwa wanaojua vizuri historia ya soka la Afrika, kwa vyovyote wataungana na mimi kwamba Simba ilikuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Klabu bingwa Afrika.

Ukiacha na historia ya Simba kufika nusu fainali ya Afrika, mwaka 1993 Simba iliingia fainali ya michuano ya kombe la CAF na ilicheza fainali na timu ya Stella Abidjan ya Ivory Coast.

Ikumbukwe michuano ya CAF imeasisi kombe la Shirikisho Afrika ikiungana na michuano ya kombe la Washindi. 
ALAMSIKI


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI