Bao lililofungwa dakika ya 54 na kiungo mshambuliaji Maxi Mpia Nzengeli raia wa DR Congo usiku huu limeisaidia timu ya Yanga SC kutinga fainali ya kombe la NBC Mapinduzi Cup uwanja wa New Amaan Stadium Zanzibar baada ya kuilaza Singida Black Stars bao 1-0.
Kwa ushindi huo Yanga itakutana na Azam FC ambao jana usiku waliifunga Simba bao 1-0 na kuwatupa nje ya mashindano hayo,
Fainali hiyo itapigwa uwanja wa Gombani mjini Pemba, bingwa wa michuano hiyo ataondoka na kitita cha shilingi milioni mia moja (100).
