Timu ya Yanga SC ya jijini Dar es Salaam jioni ya leo imeifunga bila huruma timu ya Mashujaa FC ya Kigoma mabao 6-0 mchezo wa Ligi Kuu bara inayodhaminiwa na NBC uwanja wa KMC Complex.
Mabao ya Yanga SC yamewekwa kimiani na Damaro Camaro dakika ya 07, Duke Abuye dakika ya 28, Pacome Zouzoua dakika ya 33, Prince Dube dakika ya 79 na Mudathir Yahya dakika ya 80, lingine limefungwa na Laurindo Dilson Maria Aurelio Depu dakika ya 90.
Kwa matokeo hayo Yanga SC inaongoza ligi, ikiwa na pointi 19 ikicheza mechi 7 na sasa inaelekea kujiandaa na mchezo wa kimataifa dhidi ya Al Ahly ya Misri.
.

