Klabu ya Yanga SC imetwaa taji la Mapinduzi Cup baada ya kuibuka mshindi dhidi ya Azam FC kwa mikwaju ya penalti 5–4, kufuatia sare ya bila kufungana katika muda wa kawaida na nyongeza wa mchezo wa fainali.
Mchezo huo uliisha kwa matokeo ya 0-0 ndani ya dakika 90, kabla ya kwenda kwenye dakika 30 za nyongeza ambapo hakuna timu iliyofanikiwa kupata bao.
Hata hivyo katika dakika 30 za nyongeza Yanga walikosa penalti iliyopigwa na Pacome Zouzoua na pia mchezaji wa Azam FC Diakite alioneshwa kadi nyekundu.
