Baada ya kukamilisha usajili wa golikipa Mahamadou Tanja Kassila, uongozi wa klabu ya Simba SC umeamua kumtoa Moussa Camara kwenye mfumo wa usajili ili kutoa nafasi kwa idadi ya wachezaji wa kigeni.
Uamuzi huo umechangiwa na majeraha ya goti yanayomkabili Camara, hali iliyomzuia kutoa mchango wake kwa kipindi kirefu.
Ikumbukwe kuwa mkataba wa Moussa Camara unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu, jambo linaloibua maswali kuhusu mustakabali wake ndani ya klabu.
