Naweza kufichua kuwa ofa ya Azam FC kumsajili Samba O’neil kutoka Asante Kotoko ilikuwa takriban Tsh 373,500,000 (dola za Marekani $150,000).
Kwa upande mwingine, Simba SC waliwasilisha ofa ya takriban Tsh 323,700,000 (dola $130,000).
Sijui kuhusu mazungumzo yalipofikia lakini ninachofahamu Samba ni Mcongo hivyo inaweza kuwa rahisi kwa Azam kumchukua beki huyo bora kutoka Asante Kotoko ya Ghana.
Simba wapo nyuma pia wakiendelea kusukuma kwa kuwa wanahitaji beki mgeni kwenye kikosi chao.
