Klabu ya Simba SC imeiarifu rasmi klabu ya Wydad Casablanca kuwa haina mpango wa kuendelea na huduma ya mshambuliaji Seleman Mwalimu, ambaye alikuwa akiitumikia klabu hiyo ya Msimbazi kwa mkataba wa mkopo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Simba SC imeeleza kutofurahishwa na kiwango cha mchezaji huyo, jambo lililopelekea uamuzi wa kumtaka Wydad AC kumchukua na kumrudisha klabuni kwao.
Hatua hiyo ni sehemu ya tathmini ya kikosi inayoendelea ndani ya Simba SC, ikilenga kuongeza ushindani na ufanisi katika safu ya ushambuliaji.
