Timu ya taifa ya Senegal imetawazwa kuwa mabingwa wapya wa barani Afrika baada ya kuichapa timu ya taifa ya Morocco katika mchezo mkali na mgumu wa fainali ya mataifa Afrika, AFCON.
Bao pekee lililopeleka ubingwa nchini Senegal lilifungwa na Pape Gueye dakika ya 94, ushindi huo haukuja bure, kwani Morocco walistahili ushindi hasa baada ya kupoteza penalti.
Hata hivyo wachezaji wa Senegal walikataa kuendelea na mchezo na kulazimika kutoka nje ya uwanja wakigomea penalti ya Morocco lakini shujaa alikuwa Sadio Mane aliyewashawishi wachezaji wa Senegal kuendelea na mchezo kabla hawajapata bao la ushindi.
Baadaye mshambuliaji wa Senegal Sadio Mane amechagulia na Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) kuwa mchezaji bora wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025

