Mwanaume huyu, anayejulikana kama Bwana Sinayogo Karamoko wa nchini Mali, alijitangaza kwenye mitandao ya kijamii kuwa ni mganga wa jadi mwenye uwezo wa kiroho.
Aliahidi kwamba Timu ya Taifa ya Mali itashinda AFCON 2025 (Kombe la Mataifa ya Afrika 2025). Ili kufanikisha hilo swala, aliomba michango au sadaka kutoka kwa wafuasi wake.
Alifanikiwa kukusanya zaidi ya euro 33,500 (sawa na Milioni 97.5 za kitanzania) ambazo zilitolewa na watu waliomwamini na kutarajia ushindi wa timu yao.
Hata hivyo, Mali ilitolewa nje ya mashindano katika hatua ya robo fainali baada ya kufungwa na Senegal (1-0), na kufanya utabiri huo uwe wa uongo.
Baada ya Mali kutolewa, umati wa watu wenye hasira kali ulikusanyika mbele ya nyumba yake (Bamako, mji mkuu wa Mali). Walikuwa wamekasirika sana kwa sababu ya pesa walizotoa. Polisi waliingilia kati ili kuzuia vurugu, wakamtoa nje, na kumkamata mara moja.
