Timu ya taifa ya Nigeria "Super Eagles" usiku huu wamefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali kombe la mataifa Afrika, AFCON baada ya kuilaza Algeria mabao 2-0 katika mchezo mkali na wa kusisimua.
Nigeria imekuwa katika kiwango bora na kuweza kupata matokeo mbele ya Algeria ambao walipewa nafasi kubwa ya kuvuka nusu fainali.
Mabao ya Nigeria yamefungwa na Victor Osimhen dakika ya 46 na Akor Adams dakika ya 56, kwa matokeo hayo sasa Nigeria itachuana na Morocco katika mchezo wa nusu fainali.
