Timu ya taifa ya Nigeria, Super Eagles imefanikiwa kukamata nafasi ya tatu katika michuano ya kombe la mataifa Afrika, AFCON baada ya kuifunga timu ya taifa ya Misri mabao 4-2 kwa mikwaju ya penalti kufuatia sare tasa 0-0.
Penalti ambazo zimeifanya Nigeria kuibuka washindi wa tatu zimefungwa na Adam Zakor, Moses Simon, Alex Woby na Lookman ambazo zimewafanya watwae medali ya shaba.
Nigeria ilitolewa katika hatua ya nusu fainali na timu ya taifa ya Morocco kwa mikwaju ya penalti, huku Misri nayo ikitolewa na timu ya taifa ya Senegal kwa kufungwa bao 1-0.
Kesho mchezo wa fainali utachezwa kati ya wenyeji Morocco na Senegal.
