Kiungo mshambuliaji Mzamiru Yassin amejiunga na klabu ya TRA United ya Tabora kwa mkataba wa miaka miwili akitokea klabu ya Simba SC.
Kiungo huyo alikuwa hatumiki kwenye kikosi hicho na ni uamuzi mzuri kutimka kwenye kikosi hicho kutafuta changamoto nyingine.
Mzamiru alikuwa na msimu mzuri akiwa katika kikosi cha Simba alichojiunga nacho msimu wa 2017, na amekuwa mchezaji pekee aliyedumu na Simba kwa misimu mingi zaidi kuliko mchezaji yoyote.
Mohamed Hussein Tshabalala ndiye alikuwa mchezaji pekee aliyedumu kwa kipindi kirefu zaidi lakini alitimkia Yanga mwanzoni mwa msimu huu.
