Golikipa wa zamani wa Azam FC Razak Abalora (29) kutoka Ghana sasa ni mchezaji huru baada ya kuachana na FC Zenis ya Kazakhstan.
Klabu ya Asante Kotoko inasema inamfuatilia kwa makini, huku vilabu kadhaa vya Ligi Kuu ya Ghana vikionesha nia ya kumchukua.
Abalora amekuwa na rekodi nzuri ya mafanikio, na uwezo wake uwanjani hauwezi kupuuziliwa mbali.
