Shirikisho la soka Afrika (CAF) limetangaza taarifa za droo ya mchujo wa kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika 2027, zinazotarajiwa kufanyika kesho.
Droo hiyo itashirikisha timu 12 za taifa zilizoorodheshwa chini zaidi kulingana na viwango vya hivi karibuni vya FIFA.
Raundi ya awali itachezwa katika mfumo wa mtoano, timu zikiwa zimegawanywa katika vyungu viwili.
Chungu cha 1 kitajumuisha nchi za Lesotho, Burundi, Ethiopia, Eswatini, Sudan Kusini na Mauritius.
Kwa upande wa chungu cha 2 kitakumuisha nchi za Chad, Sao Tome na PrÃncipe, Djibouti, Somalia, Shelisheli pamoja na Eritrea.
Mashindano ya AFCON mwaka ujao yamepangwa kufanyikia Tanzania, Kenya na Uganda, maandalizi yakiendelea kufanyika hasa ujenzi wa Viwanja na miundo mbinu mingine.
