Bado kampuni ya DPWORLD iliyoichukua Bandari ya Tanzania kwa uwekezaji wa kupokea na kusafirisha makontena inaendelea kuitaka klabu ya Simba SC Ili iichukue na kuwa Mdhamini mkuu.
Taarifa za ndani zinasema DPWORLD itawamwagia fedha nyingi Simba SC kwakuwa itawatangaza kimataifa katika biashara zao za bandarini.
DPWORLD hawataki kuwa wadhamini wenza wakishirikiana na MO Dewji, isipokuwa kampuni hiyo inataka kuwa wadhamini wakuu, na suala la fedha ndio basi tena.
Simba mpaka sasa inasuasua katika kufanya usajili wachezaji mahiri na ndio maana timu haifanyi vizuri, lakini ujio wa DPWORLD unaweza kuondoa shida zote.
