Serikali ya Gabon imesitisha shughuli za timu ya taifa hadi taarifa nyingine itakapotolewa, kufuatia kile ilichokitaja kuwa ni “kiwango kibovu” katika AFCON 2025, baada ya taifa hilo kutolewa mapema katika hatua ya makundi.
Aidha, nahodha Bruno Ecuele Manga pamoja na Pierre-Emerick Aubameyang wamepigwa marufuku ya kuichezea timu ya taifa ya Gabon.
