Ingawa ajapata nafasi ya kucheza mara kwa mara kwenye kikosi cha kwanza cha Yanga, mshambuliaji Andy Boyeli aliyetupiwa virago amewashuruku mashabiki, viongozi na wachezaji wenzake kwa kumuonesha upendo wa hali ya juu.
"Sijapata nafasi ya kucheza mara kwa mara, lakini nimeonyeshwa upendo mkubwa kuanzia viongozi wachezaji na hata mashabiki wa Yanga SC, wana upendo mkubwa mno wataendelea kuishi moyoni mwangu.
Licha ya changamoto ya kushindwa kufanya kile walichokuwa wanatarajia kutoka kwangu hawakuwahi kuniacha, walikuwa pamoja nami walinipa imani na nguvu ya kupambana zaidi ni furaha kufanya kazi nao"
Andy Boyeli, Mshambuliaji wa zamani wa Yanga SC.
