Mwaka 2025 umekua Mwaka Bora sana kwangu Binafsi.
Nimevaa jezi ya Taifa Stars kwa fahari kubwa, nikapigania bendera ya Tanzania kwa damu, jasho na moyo wote na kuwa sehemu ya historia ya kufuzu Hatua ya 16 Bora AFCON na Robo Fainali CHAN kwa mara ya kwanza tangu Taifa letu lipate Uhuru.
Kwa Wananchi wenzangu Yanga tumepigana hadi mwisho, tukatengeneza historia kwa kutwaa Ligi Kuu, Kombe la FA na Ngao ya Jamii. Kila jasho langu uwanjani mwaka huu lilikuwa ahadi kwa mashabiki, kila ushindi ulikuwa sauti yenu Wananchi.
Mafanikio ya 2025 siyachukulii kama mwisho, Ni deni la kunyoosha zaidi 2026.
Kwaheri 2025 ya Historia,
Heri ya Mwaka Mpya Tanzania 2026
