Taarifa kutoka TFF zinasema, licha ya Hemed Suleiman Ali Morocco kutolewa katika nafasi hiyo ya kuinoa timu ya taifa, Taifa Stars, Shirikisho hilo litampeleka nje ya nchi kuongeza ujuzi zaidi.
Kiongozi mmoja wa TFF amesema kuwa, sio Morocco peke yake, wapo makocha wengine ambao watapata fursa hiyo ya kwenda kujiendeleza zaidi kisha kuja kupewa timu za taifa hapo baadaye.
