Taarifa ya Simba kushtakiwa CAF ni kweli na waliopeleka kesi hiyo ni Nsingizini Hotspurs kwa kosa la Simba kumruhusu kocha wao Dimitar Pantev kukaa kwenye Touch line ikiwa hana vigezo vya kukaa hapo.
Simba walimtambulisha Pantev kama meneja mkuu na sio kocha na nafasi ya ukocha mkuu alipewa Seleman Matola ambaye miaka yote amekuwa msaidizi kwenye kikosi hicho.
Inasemekana Pantev hana vigezo vya kumfanya awe kocha mkuu wa klabu hiyo kwa sababu ana leseni ya UEFA ambayo haimfanyi kukaa kwenye touch line
