Baada ya kuzuka kwa taarifa kuwa Mchezaji wa Yanga Aziz Andabwile amefungua kesi ya madai TFF akioshitaki klabu yake ya Yanga kwa kutokumlipa fedha zake za usajili hadi Leo
Mchezaji huyo kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika ujumbe wa kukanusha taarifa hizo na kuwataka waandishi wa habari kupata habari kutoka kwa vyanzo vya uhakika
Andabwile ameandika
"Habari Wananchi. Nipende kuchukua nafasi hii kuliweka sawa jambo linaloendelea mtandaoni kuhusu mimi na Klabu yangu ya Yanga.
Mimi ni mchezaji wa Young Africans Sports Club na haki zangu za kimkataba tayari nilishalipwa.
Niwaombe ndugu waandishi wa Habari kuwa na vyanzo sahihi vya taarifa ili kutoleta taharuki kwa wachezaji kwenye Timu zao
Mwisho, niwaombe radhi wote ambao wamekwazika na sintofahamu iliyojitokeza.
