Aliyewahi kuwa nyota wa Mbao na KMC,Yusuf Ndikumana raia wa Burundi amejiunga na klabu ya TRA United yenye maskani yake mkoani Tabora kama kocha wa viungo na utimamu wa mwili.
Ndikumana anaungana na aliyewahi kuwa kocha wake wakati anasakata kabumbu,Ettiene Ndayiragije ambaye amejiunga pia na TRA kama kocha mkuu baada ya kuachana na klabu ya Police ya Kenya.
Ndikumana ameachana na Dodoma Jiji ambapo alikuwa akihudumu katika nafasi kama ambayo anaenda kuitumikia TRA hivi karibuni na kujiunga na wakusanya mapato.
