Anaandika George Ambangile
Kila nikijitahidi kuamini kama zama za Aishi Manula zimekwisha kwenye soka la Tanzania moyo wangu unakua mzito kulipokea jambo hili naona kama ni mapema sana kwa sababu mbadala halisi wa kipa huyu bado hajapatikana.
Baada ya kufungwa mabao matano na Young Africans Sc ni kama Simba Sc waliamua kumgeuzia kisogo na kumtoa kwenye ramani ya soka kabisa Ila madhara makubwa yanatokea kwenye timu ya taifa ya Tanzania.
Naheshimu uteuzi wa makipa wanaoitwa timu ya taifa, lakini ule ukomavu, uzoefu na ubora alionao Aish Manula bado haujaanza kuonekana labda niseme ni papara au haraka zangu Ila hawa makipa walipaswa kujifunza zaidi mbele ya Manula.
Makipa wa sasa makosa yao yamekua mengi na tena ya kujirudia tunaenda Afcon nchini Morocco ni heri benchi la ufundi Kuliangalia jambo hili mapema japo naheshimu maamuzi yenu na timu ya taifa ni timu ya wachezaji wote.
Uganda waliamua kufanya maamuzi magumu kumrejesha Dennis Onyango timu ya taifa wanajua kabisa wanaenda kwenye mashindano ya Afcon na wanaona bado kuna mchango Onyango anaweza akautoa timu ya taifa.
Kipa mkomavu mzawa kama Manula ambaye amecheza mashindano makubwa kwa ngazi ya vilabu na timu ya taifa bado hayupo kumbuka kuna muda alikua anapunguza idadi kubwa ya magoli nan anakumbuka mechi ya Nigeria na Tanzania kule nchini Nigeria, Simba na Asec Memosas kule Ivory Coast kwa kupangua penati 2.
Jambo hili linaweza kutuumiza wenyewe wakati bado tuna nafasi ya kufanya maamuzi sahihi na kwanini waliamua kumuita Tanzania one wakati kuna makipa wengi kwenye ligi Yetu.
Kwa sasa hatuna kipa mzawa na mwenye upekee kama Aish Manula narudia tena ubora, ukomavu, uzoefu na uongozi wake kiwanjani ni unakosekana na unahitajika kwa kiasi kikubwa.
Nembo ya makipa wazawa kwa sasa tunaamua kuipoteza wenyewe muda bado upo wa kufanya maamuzi na umri wake bado unaruhusu.
