Meneja mkuu wa klabu ya Simba SC Dimitar Pantev raia wa Burgalia, ametoboa kilichomfanya asimuamzishe mshambuliaji halisi wa kusimama na kupelekea kumuanzisha mshambuliaji wa uongo.
Malalamiko yamezidi kumuelemea yeye baada ya jana Simba kufungwa bao 1-0 na Petro de Luanda ya Angola mchezo wa Ligi ya mabingwa Afrika uwanja wa Mkapa ambapo meneja huyo alimpanga Elie Mpanzu kama mshambuliaji wa kusimama mbele badala ya Stephen Mukwala au Jonathan Sowah.
Akizungumza baada ya mchezo huo, meneja huyo amesema kama ifuatavyo:
“Tuliwatazama vyema wana mabeki wawili wa kati wazuri sana ambao tungeanza na namba 9 ya kusimama wangeweza kumdhibiti kirahisi sana, ndio maana tukaona tuanze na tisa kivuli ili kutuongezea mtu kwenye kiungo, bila shaka mliona kipindi cha kwanza tulicheza vizuri sana", alimsliza.
