Huyu Mwamba leo hamna rangi ataacha kuona, ila sometimes Wachezaji wana nafasi ya kuwajibika zaidi ya Kocha, Simba wangekua wafanisi kwa nafasi zilizo dondoka kwao first half game ilitakiwa kua isha isha
Ibraham yeye na goli, Mpanzu yeye na goli~ hizo ni nafasi mbili ambazo Mpanzu na Abraham wange lenga tuu goli kipa wa Petro asinge weza kuzuia, alafu kuna nusu nafasi zilizo dondoka kwa Mutale na Rushine
Team ikitengeneza nafasi wakwanza kutakiwa kuwajibika ni mchezaji alafu ndio mengine yata fatia...
Na nawaelewa watakao Mlaumu Pantev, kwenye nafasi zote zilizo potezwa kama izo nafasi zinge dondoka kwa Sowah ama Mwalimu, mpira unaukuta nyavuni
Anaandika Mchambuzi wa soka Khalfani kutoka #Wasasfifm
