Klabu ya KMC FC imefikiria kumpa mkono wa kwaheri kocha wao mkongwe Marcio Maximo, kutokana na mwendelezo mbovu klabuni humo.
Kwa mujibu wa taarifa za kuaminika kutoka ndani ya klabu hiyo, zinasema kocha huyo tayari amepewa idadi ya michezo na watakaanae kikao kizito weekend hii endapo atapoteza mchezo wake dhidi ya Yanga kujua kuhusu kibalua chake.
KMC FC wamekuwa na wakati mgumu kwenye Ligi msimu huu licha ya kushinda mchezo wa kwanza dhidi ya Dodoma Jiji lakini wamepoteza michezo yote iliyofuata na mpaka sasa wana alama tatu pekee wakiwa nafasi ya 16 katika msimamo wa Ligi hiyo.
