Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limemteua Meneja wa Mashindano wa TFF, Baraka Kizuguto, kuwa Mrakibu Mkuu (General Coordinator) wa michezo ya nusu fainali ya hatua za awali za kufuzu Kombe la Dunia Kanda ya Afrika (Play-Off Tournament) kati ya Nigeria na Gabon, pamoja na mchezo wa fainali.
Michezo hiyo itachezwa Rabat, Morocco tarehe 13 na 16 Novemba 2025.
