TIMU ya JKT Queens imetoa sare ya bila mabao na Gaborone United ya Botswana katika mchezo wa Kundi B Ligi ya Mabingwa Afrika Wanawake usiku huu Uwanja wa Suez Canal Jijini Ismailia nchini Misri.
Mchezo uliotangulia wa ufunguzi wa Kundi B pia, ASEC Mimosas ya Ivory Coast imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya mabingwa watetezi, TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) hapo hapo Uwanja wa Suez Canal, Ismailia.
Ikumbukwe jana zilichezwa mechi za ufunguzi wa jumla za michuano hiyo ambazo zilikuwa ni za Kundi A na wenyeji, FC Masar ya Misri walilazimishwa sare ya bila mabao na AS FAR Rabat ya Morocco hapo hapo Suez Canal.
Mechi nyingine ya Kundi A iliyotangulia jioni ya jana Uwanja wa Suez Canal — USFAS Bamako ya Mali iliichapa FC 15 de Agosto ya Angola mabao 2-1.
