Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Bw. Gerson Msigwa, amerejea na tuzo aliyopewa Rais Samia Suluhu Hassan, Novemba 19, 2025 na Shirikisho la Mpira Barani Afrika (CAF), kwa kutambua mchango wake mkubwa katika maendeleo ya Mpira nchini.
Msigwa, alipokea tuzo hiyo kwa niaba ya Rais Samia, mjini Rabat nchini Morocco.
