George Mpole, aliyewahi kung’ara Geita Gold na Pamba Jiji na kucheza nje ya nchi, amevunja ukimya akifichua kuwa alikuwa akifanya majaribio ndani ya takriban wiki tatu na klabu ya Siwelele F.C ya Ligi Kuu Afrika Kusini.
Amesema amerudi nchini akisubiri dili huku akisisitiza mpira ni kazi yake na anaendelea kujipa ubora akiwa nje ya timu.
