Klabu ya Singida Black Stars imetangaza kuchagua kuutumia uwanja wa New Amaan-Zanzibar kwenye mechi zao za nyumbani kwenye mechi za hatua ya Makundi Kombe la Shirikisho Afrika 2025/26.
Singida Black Stars imefuzu hatua ya Makundi ya michuano hiyo kwa mara ya kwanza, na sasa inasubiri droo ya kupanga makundi itakayofanyika Johannesburg, South Africa Jumatatu ijayo Novemba 03,2025
