Klabu ya Pamba Jiji imepewa alama tatu na magoli matatu baada ya mchezo wao dhidi ya Dodoma Jiji kushindwa kuendelea ukichezwa dakika 6 tu.
Mchezo huo ulindwa kuendelea kutokana na umeme kukatika dakika ya 6, hivyo kamati ya uendeshaji na usimamizi wa ligi ya bodi ya ligi kuu (TPLB) imewapata Pamba alama tatu na magoli matatu kwa kosa la wenyeji (Dodoma Jiji) kushindwa kuuandaa mchezo vyema.
