MWENYEKITI wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Stephen Mnguto amewasilisha barua ya kujiuzulu wadhifa wake – huku Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia akimsimamisha kazi Mtendaji Mkuu wa TPLB, Almasi Kasongo.
Taarifa fupi mno iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao imesema kwamba Mnguto amejiuzulu na Karia amemsimamisha kazi Kasongo.
Hatua hii inakuja wakati inafahamika Yanga iliwasilisha matakwa manne yakiwemo kujiuzulu kwa Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi, Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Almasi Kasongo ajiuzulu na Katibu Mkuu mwenyewe wa TFF, Kidao — na la nne ambalo ni la muda mrefu nyundo mpya wa Bodi Huru ya Ligi.
Yanga ilitoa masharti hayo na ikishurtisha yatimizwe ndio wacheze mchezo wa marudiano wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara dhidi ya mahasimu, Simba ambao sasa umepangwa kufanyika Juni 25 Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

