Nyota imeendelea kung'aa Kwa mshambuliaji wa klabu ya Wydad Casablanca na Timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Selemani Mwalimu "Gomez" mara baada ya kuingia makubaliano na Kusaini mkataba na Kampuni maarufu Duniani la Skechers ambalo Limesaini mkataba na baadhi ya mastaa wa kubwa barani ulaya
Mara baada ya Kusaini mkataba huo Mwalimu atakuwa akivaa viatu na nguo zenye nembo ya Kampuni la Skechers ambayo inawavalisha baadhi ya mastaa wakubwa Duniani ikiwemo mshambuliaji Wa Klabu ya Bayern Munich, Harry Kane na kiungo Mshambuliaji Wa klabu ya West Ham United, Mohamed Kudus.