“Madhara ya kushuka daraja kwa timu tusikubali yaingie Ruangwa, mtakuja kunikumbuka, ligi kuu ina mchango mkubwa kwenye hamasa tuliyonayo Ruangwa na maendeleo ya Ruangwa ikishuka hakutokuwa na hamasa.
Huwezi kutembea kifua mbele, leo Yanga wanakuja hapa, Simba, Singida BS, Kagera Sugar, Mashujaa wote wanakuja hapa na wakija wanaiongezea thamani ya Ruangwa, leo Wana Ruangwa tunaungwa mkono na Watu wa Nachingwea na Lindi wanakodi mabasi wanakuja kushangilia timu yetu.
Namungo isishuke daraja, tuichangie hii timu, kuifanya timu kuwa ligi kuu kuna gharama kubwa”
“Timu kubaki ligi kuu kuna faida zake huwezi kuiona haraka haraka, ikiondoka ndio utajua, uliza Watu wa Mtwara na timu yaonya Ndanda leo wanasema nini?.
Kila vikao wakikaa havikaliki hakuna masuluhisho na wameshindwa kuifanya ile irudi tena, ikishuka kurudi ngumu, Lindi imeshuka timu ya Kariakoo mpaka leo tunahangaika Lindi Mjini mwisho juzi imekuja timu hata haielewi, bado haijaeleweka”
“Mtu ametoka na timu yake huko amenunua yeye ya kwake ameileta Lindi, Wana Lindi wanaiangalia wanaona kama sio ya kwao, Namungo ni yetu ameanzisha Mama Mpemba na Mumewe na ikaanza kucheza na Vijana wetu wanaochimba madini ile ni ya kwetu”
