Taarifa za kuaminika ni kuwa winga wa Orlando Pirates, Karim Kimvuidi hataondoka klabuni hapo baada ya msimu wa PSL kumalizika
Winga Kimvuidi ataendelea kupambania namba katika kikosi cha Orlando Pirates na ni jambo ambalo imekuwa changamoto kubwa kwake.
Meneja wa Karim Kimvuidi alikuwa akimsisitizia mteja wake ashinikize kuondoka licha ya Kimvuidi bado ana mkataba na Orlando Pirates lakini viongozi wa Orlando Pirates wamemshauli winga huyo abaki na amekubali kupambania namba
Karim Kimvuidi anahusishwa kuhitajika na klabu ya Simba SC ikiwa Karim Kimvuidi atamalizana na Orlando Pirates katika dirisha kubwa lijalo la uhamisho.
