Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya kimataifa Simba SC jioni ya leo imenusa fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya kuifunga Stellenbosch ya Afrika Kusini bao 1-0 uwanja wa New Amaan Stadium Zanzibar.
Bao pekee la Simba ambalo lilizua tafrani kiasi kwamba VAR ilitumika kuamua kama ni goli au lah! Lilifungwa na Jean Charles Ahoua dakika ya 45.
Simba sasa inahitaji kulinda goli kwenye mchezo wa marudiano utakaofanyika Aprili 27 wiki ijayo mjini Dublin Afrika Kusini, mshindi wa mechi hiyo atakutana na CS Constantine au RS Berkane.
Hata hivyo katika mchezo huo Simba itabidi ijilaumu yenyewe baada ya kukosa goli la wazi kupitia Ahoua.
