Klabu ya Orlando Pirates imethibitisha kuwa kocha wao Mkuu Raia wa Hispania Jose Riveiro ataondoka klabuni ifikapo mwishoni mwa msimu huu,
Orlando Pirates ipo kwenye msimu bora kwenye michuano ya CAFCL ambao katika mechi ya kwanza ya Robo Fainali walishinda bao 1-0 wakiwa ugenini dhidi ya MC Alger.
Kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Afrika Kusini, ipo kwenye mbio za ubingwa ikishika nafasi ya pili nyuma ya Mamelodi Sundowns ambao ni vinara.
Imeelezwa kuwa kocha huyo amepata ofa kubwa kutoka Saudi Arabia.
