Klabu ya Fountain Gate imemfuta kazi aliyekuwa kocha wao Mkuu Raia wa Kenya Robert Matano.
Huku ikifahamika maelewano mabaya baina yake na Wachezaji na Viongozi klabuni hapo ndio sababu ya kuachana nae.
Kwasasa kikosi cha Fountain Gate kipo chini ya Kocha wa zamani wa klabu ya Mwadui Khalid Adam 'kibonge' ambaye anasaidiana na Amri Said 'Stam'.
Rekodi za Matano
Robert Matano raia wa Kenya, huyu ndio kocha mwenye mafanikio makubwa zaidi kwa makocha raia wa Kenya kwenye ligi ya nchini Kenya ametwaa mataji manne ya ligi kuu nchini humo akiwa na timu tofauti tofauti.
Amebeba akiwa na Sofapaka 2009, Tusker Fc 2012,2020/21 na 2021/22.
Matano ni shabiki lialia wa Simba Sc toka kipindi hicho anatwanga mbungi
