MSHAMBULIAJI wa Yanga, Prince Dube ndiye anayeongoza kwa kufunga mabao mengi zaidi ya kichwa msimu huu katika Ligi Kuu Bara, baada ya kufunga sita kati ya 12 aliyofunga, akiwa sambamba na kiungo mshambuliaji wa Simba, Jean Charles Ahoua.
Wengine wanaofuatia kwa kufunga mabao mengi zaidi ya kichwa ni Heritier Makambo wa Tabora United aliyefunga manne, huku Ibrahim Hamad 'Bacca' wa Yanga na Elvis Rupia wa Singida Black Stars, kila mmoja wao akitupia kambani matatu hadi sasa.
