Anaitwa Cindy Kakolanya mwanadada anayefanya vizuri kwenye series ya DUNIA.
Cindy anatisha na ni miongoni mwa wasanii wanaovutia hapa nchini kwani katika series hiyo anacheza kama mwanamke mwenye upendo akianza kwa Mudy Muzungu paka la bar na baadaye mtumishi Amani.
Cindy alikosa furaha kwa Mudy Kwa sababu ni chapombe hivyo hawezi kumpa mapenzi shata shata, ila upendo ataupata kwa Amani ingawa Amani ni muoga anaogopa mume wa mtu na pia makatazo ya Imani yake ya ulokole.
Kwa kifupi Cindy anaingia kwenye orodha ya mastaa wanaokuja kutikisa hapa nchini na Afrika mashariki kwa ujumla.

