Wekundu wa Msimbazi, Simba SC wameichapa Namungo FC mabao 3-0 katika uwanja wa Majaliwa Stadium Ruangwa Lindi mchezo wa Ligi Kuu bara na kufikisha pointi 50 ikiwa nafasi ya pili nyuma ya Yanga.
Hata hivyo mwamuzi wa mchezo huo amewaua Namungo wazi wazi kwa kuwapa penalti tatu Simba na pia kumpa kadi nyekundu mchezaji wa Namungo bila kosa la msingi.
Mabao mawili ya Simba yamefungwa kwa mikwaju wa penalti na Jean Charles Ahoua dakika ya 45 na 70 wakati goli la tatu limefungwa na Stephen Mukwala dakika ya 90
