Klabu ya Simba ilituma ofa ya USD 200,000 katika klabu ya Rivers United ikihitaji saini ya kiungo wa ulinzi, Augustine Okejepha lakini ofa hiyo imekataliwa.
Rivers United wanahitaji USD 270,000 kutoka klabu ya Simba ili kumuachia Augustine Okejepha ambaye amekuwa na msimu bora sana katika michuano ya kimataifa ya CAF msimu uliopita na Ligi Kuu ya Nigeria.
Lakini pia Rivers United wamepewa taarifa na klabu moja kutoka Ubelgiji kuwa itatuma ofa kwao wiki ijayo ili kupata huduma ya Augustine Okejepha na klabu ya Rivers United ipo tayari kusubiri ofa hiyo.
