Nyota wa klabu ya Medeama ya Ghana Derrick Fordjour ambaye ameripotiwa na vyombo vya habari nchini Ghana kuwa yupo mbioni kutua Msimbazi kwenye dirisha kubwa lijalo la usajili huku tayari akiwa amewatumikia Medeama kwa msimu wa pili mpaka sasa ambapo amejiunga na klabu hii kwa mkataba wa miaka 4 mwaka 2022.
Hizi hapa ni takwimu za mchezaji huyu akiwa na Mediama,
Msimu wa 2022/2023 nyota huyu alicheza jumla ya michezo 27 huku akifunga jumla ya mabao 2 na kutoa pasi za mwisho 5 na kuisaidia Mediama kutwaa kombe la ligi kuu Ghana.
Msimu wa 2023/2024 mpaka sasa tayari amecheza jumla ya michezo 19 na amefunga bao 1 tu.
